Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Taaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam anapenda kuwataarifu
Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe Machi 8, 2025 na
hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.Wasailiwa wanaoitwa kwenye
usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
1. Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili muda na sehemu ambapo
usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.
2. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
3. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga
kura,Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria.
4. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI,
Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji.
5. Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hati za
matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA
HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
6. Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
7. Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
8. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na
Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA)
9. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi
vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya
tangazo husika.
10. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti
vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.
11. Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba
ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa siku ya usaili
More Information
- Address Dar es Salaam
- Announcement type Call for Interviews
- View File Here 20252302511845TANGAZO-LA-USAILI-UDSM.pdf